
KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA.
WARAKA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wanachama wake
kushinikiza watetea matakwa ya chama hicho kwenye maoni yao katika
mchakato wa Katiba Mpya umezua balaa, baada ya Mjumbe wa Tume ya Katiba
kumzuia mmoja wa wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya kutumia waraka huo kutoa
maoni yake.
Alhaj Siad Elmamri ambaye kitaalamu ni
mwanasheria, alimzuia Hussein Kiswil aliyekuwa akichangia mapendekezo
kwenye rasimu hiyo, baada ya kubaini kuwa, alichokuwa anazungumza
kilitokana na maelekezo ya CCM.
Hata hivyo hatua hiyo ilizua tafrani katika
mkutano huo, baada ya mjumbe huyo wa baraza la Katiba wilaya,
kutoridhika na msimamo huo wa mjumbe wa tume na kupend
ekeza afukuzwe kwenye mchakato huo, kwa kile alichoeleza kuwa anapingana na maelekezo ya kuwaacha watu watoe maoni yao kwa uhuru.
ekeza afukuzwe kwenye mchakato huo, kwa kile alichoeleza kuwa anapingana na maelekezo ya kuwaacha watu watoe maoni yao kwa uhuru.
Kiswil alidai kuwa mjumbe huyo hastahili kuendelea
na kazi ya kusimamia mabaraza hayo kwa kuwa yeye pamoja na wajumbe
wenzake kadhaa, hawana imani naye.
“Siku ya jana (juzi) tukiwa ndani ya ukumbi huu
mlitueleza kuwa kila mtu anayo haki ya kutoa maoni yake katika kuchangia
Rasimu ya Katiba hii, mimi nilichaguliwa kuingia katika kundi na kupewa
jukumu la kuchambua muundo Muungano” alisema Kiswil na kuongeza;
“Nilipoanza kuchangia mimi aliingia Mjumbe wa tume
Elmamri na kusikiliza, nilipomaliza kabla hata ya kuruhusiwa na
mwenyekiti alianza kuzungumza akisema maoni niliyotoa mimi ni maelekezo
ya Chama Cha Mapinduzi na aliongeza kuwa ana taarifa za kuwapo kwa
kiongozi mkubwa wa kisiasa aliyekuja Iringa kutoa semina… nilitaka
anithibitishie kama hayo aliyoyasema ni ya kweli.”
Alisema kufuatia hatua hiyo ya mjumbe kushindwa
kuthibitisha juu ya kuwapo kwa maelezo hayo kutoka CCM na suala la ujio
wa kiongozi mkubwa wa CCM ngazi ya Taifa kuja kutoa semina alipendekeza
kikao hicho cha Baraza la Katiba kujadili hoja hiyo aliyotoa na kutolea
maamuzi.
Akizungumza mara baada ya kupatiwa nafasi na
mwenyekiti wa kikao hicho Omary Shahe Mussa, Elmamri alikiri kutoa
ushauri kwa wajumbe kutumia nafasi hiyo kuchangia maoni yao badala ya
maoni na msimamo wa chama.
Alisema alitoa ushauri huo kufuatia kusoma kwake
habari kutoka katika gazeti la Mwananchi iliyoelekeza maoni na msimamo
wa Chama Cha Mapinduzi katika rasimu hiyo na kufafanua kuwa hata mjumbe
alitoa yale yaliyokuwa yameshaandikwa na gazeti hili.
“Mwenyekiti waTume Jaji Mstaafu Joseph Warioba
alionya juu ya wanasisa kuacha wananchi kutoa maoni yao na alisisitiza
kuwa vyama vya kuchangia maoni yao binafsi na si kutoka kwa viongozi wa
vyama na kuongeza kuwa alifanya hivyo kutokana na msimamo
uliokwishatolewa na Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Joseph Warioba.
Wiki iliyopita, gazeti hili liliripoti habari za
CCM kusambaza waraka kwa wanachama wake ambao ni Wajumbe wa Mabaraza ya
Katiba ngazi ya wilaya, kutaka wakisaidie chama hicho katika kutetea
hoja zake kwenye mchakato wa Katiba Mpya.
Pamoja na mambo mengine, chama hicho
kimetofautiana na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu Muundo wa
Muungano, baada ya kupendekeza Muungano wa Serikali mbili badala ya
serikali tatu. MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment