Juma Mtanda, Morogoro.
Timu ya soka ya Kinglwira FC imeishushia mvua ya mabao Kihonda Star katika muendelezo wa ligi daraja la nne msimu wa mwaka 2015/2016 kwa kuicharaza bao 3-0 katika mchezo mkali uliofanyika jana kwenye uwanja wa Sabasaba mkoani Morogoro.
Mshambuliaji wa Kinglwira FC, Nurdin Nurdin ndiye aliyeonekana mwiba mchungu kwa timu ya Kihonda Star kwa kufunga bao mbili pekee katika dakika ya 82 na 90 kufuatia pasi za mwisho za wachezaji Mohamed Mnyepe na Salum Nzange.
Nurdin alifunga mabao hayo moja akifunga kwa tiktaka baada ya mpira wa kona ulioanzishwa na Omari Godfrey kisha kukumiminwa krosi iliyomkuta mfungaji kabla ya kupokea pasi ya Salum Nzange.
Bao la kwanza la Kinglwira lilifungwa na Mohamed Mnyepe dakika ya 43 huku Kihonda Star ikishindwa kufurukuta mbele ya wapinzani wao katika mchezo huo.
Katika michezo mingine timu ya Moro Youth FC ilitembeza kipigo kwa timu ya G-Seven baada ya kuisambaratisha kwa bao 4-1 wakati Don Bosco FC na Uluguay ya Sultan zikishindwa kutambiana baada ya sare ya bao 1-1.
Timu ya Maskan FC yenyewe ilikubali kutandikwa bao 1-0 mbele ya Barafu FC ya Kihonda na Magadu FC na Lubungo FC zilishindwa kucheza mchezo wao Desemba 26 ikipisha ligi daraja la kwanza kwa mchezo baina ya Polisi Moro SC na Burkina katika mchezo uloisha kwa sare ya bao 2-2.
Katika mchezo huo kati ya Magadu FC na Lubungo FC utachezwa januari mosi ambapo katika mchezo wa leo (jana) Moro City FC itaonyesha umwamba na Chipolopolo FC saa 10 jioni katika uwanja wa Sabasaba.CHANZO:MTANDA BLOG
Wednesday, December 30, 2015
KUTOKA KWENYE MAGAZETI YA HARDNEWS JUMATANO DECEMBA 30/ 2015 YAKIWA NA VICHWA VIKUU VYA HABARI

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.
Subscribe to:
Comments (Atom)






